Mkurugenzi wa shule hiyo, Sheikh Shafi Nina, alieleza kufurahishwa kwake na ziara hiyo, akiitaja kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha mahusiano na taasisi za kitaifa na kimataifa kwa ajili ya mafanikio ya Kisayansi kwa vijana wa Kitanzania.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA -Leo tarehe [08, 05,2025], Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam, Dkt. Ali Taqavi, alifanya ziara rasmi katika Shule ya Abul Fadhli Al-Abbas (as) iliyopo Tanga Mjini.
Akiwa ameambatana na Sayyid Arif Naqvi, Mkuu wa Taasisi ya Hojjatul Asr Foundation - Tanzania, walipokelewa na uongozi wa shule hiyo kwa mapokezi mazuri na ya heshima.
Katika ziara hiyo, viongozi hao walipata fursa ya kukutana na uongozi wa shule na kufanya mazungumzo muhimu kuhusu maendeleo ya kielimu na changamoto mbalimbali.
Walitembelea maeneo mbalimbali ya shule, wakajionea shughuli za kila siku, ikiwemo vipindi vya masomo, vitendo vya idara, na shughuli za kimaendeleo zinazotekelezwa na shule hiyo.
Pia walishuhudia vifaa mbalimbali vya kisasa vinavyotumika katika kusaidia utoaji wa elimu bora katika mazingira safi, salama, na yanayowavutia wanafunzi kujifunza kwa ari na bidii.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Sheikh Shafi Nina, alieleza kufurahishwa kwake na ziara hiyo, akiitaja kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha mahusiano na taasisi za kitaifa na kimataifa kwa ajili ya mafanikio ya Kisayansi kwa vijana wa Kitanzania.
Aidha, alitoa ripoti ya kina ya maendeleo ya shule hiyo, ikiwa ni pamoja na mafanikio ya wanafunzi kitaaluma na kijamii.
Your Comment